DAR-Aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania 2025 kupitia Chama cha CHAUMMA na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu amesema kuwa,ana imani kubwa na Tume ya Jaji Chande inayochunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Salum amesisitiza kuwa,tume hiyo ni ya Watanzania wote,kwani inakwenda kutibu majeraha yaliyokotea na amesisitiza umuhimu wa maridhiano pale ambapo tume hiyo itakuwa imetoa majibu yake.
