ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na uongozi wa Benki ya Ecobank, ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Biashara na Uwekezaji kutoka makao makuu ya benki hiyo nchini Togo, Bw. Michael Larbie, aliyefuatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Ecobank Tanzania, Ndugu Charles Asiedu leo Aprili 15,2026 Ikulu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Akiwa na Bw. Michael Larbie Afisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Biashara na Uwekezaji kutoka Makao Makuu ya Benki hiyo Nchini Togo, Ikulu ya Zanzibar, leo Aprili 15, 2026.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Akiwa na Bw. Michael Larbie Afisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Biashara na Uwekezaji kutoka Makao Makuu ya Benki hiyo Nchini Togo, Ikulu ya Zanzibar, leo Aprili 15, 2026.Katika mazungumzo hayo, Rais Dkt. Mwinyi ameishukuru Ecobank kwa kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kuunga mkono juhudi za maendeleo ya kiuchumi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Ecobank kutoka Nchini Togo, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo Aprili 15, 2026, Ikulu Zanzibar.Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameihakikishia benki hiyo ushirikiano endelevu, huku akibainisha fursa mbalimbali za uwekezaji, ikiwemo bandari, miundombinu ya barabara na uchumi wa buluu.
Kwa upande wake, Bw. Michael Larbie amesema Ecobank itaendelea kushirikiana na Zanzibar na kuimarisha ushirikiano wa kifedha na kibiashara barani Afrika kupitia mpango wake wa Pan African Partnership.


