Rais Dkt.Mwinyi atoa salamu za pole kifo cha Mstahiki Meya mstaafu wa Jiji la Zanzibar

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mstahiki Meya mstaafu wa Jiji la Zanzibar, Mahmoud Muhammed Mussa, kilichotokea Aprili 6, 2026 nyumbani kwake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.(Picha na Maktaba).

Katika salamu zake, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kusikitishwa na taarifa za kifo hicho, akibainisha kuwa Taifa limepoteza kiongozi shupavu, mzalendo na mtumishi mahiri wa umma.

Amesema, marehemu Mussa alitoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Jiji la Zanzibar na katika kuimarisha misingi ya utawala bora kupitia nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika serikalini na ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Aidha, Rais Mwinyi amekumbusha kuwa marehemu aliwahi kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, pamoja na majukumu mengine ya uongozi yaliyomjengea heshima na kutambuliwa na jamii.

Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wake, Rais Mwinyi ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki, akiwataka kuwa na subira na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

“Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,” amesema Rais Mwinyi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here