ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameondoka Unguja leo tarehe 02 Aprili 2026 na kuwasili Pemba kushiriki Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, katika Uwanja wa Gombani, Mkoa wa Kusini Pemba.
Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Pemba, amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.



