Dkt.Mnyepe aongoza ujumbe wa Tanzania mkutano wa 13 wa amani,ulinzi,usalama na sera za mambo ya nje EAC

NAIROBI-Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Mnyepe ameongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 13 wa Pamoja wa Mabaraza ya Kisekta ya Mawaziri wa Ushirikiano katika Ulinzi, Amani na Usalama na Baraza la Kisekta la Uratibu wa Sera za Mambo ya Nje, ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika jijini Nairobi, Kenya, Aprili Mosi 2026.
Mkutano huo ulijadili Taarifa ya Utekelezaji wa Maamuzi yaliyopita ya Baraza hilo, hatua iliyofikiwa katika uandaaji wa Mfumo Jumuishi wa Tahadhari ya Mapema, kupitia Rasimu ya Mpango Mkakati wa Ushirikishwaji wa Wanawake katika Amani, Ulinzi na Usalama wa EAC na kupitia Mpango Mkakati wa Ushirishwaji wa Asasi zisizo za kiserikali katika uzuiaji, usimamizi na utatuzi wa migogoro katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Aidha, Makatibu Wakuu hao pia wamefanya mapitio ya Utekelezaji wa Programu ya uelimishaji wa Jamii zinazoishi mipakani kuhusu ujirani mwema na masuala ya usimamizi wa mipaka.

Manaibu Katibu Wakuu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi : Balozi Said Shaib Mussa na Dkt. Maduhu Kazi, wameshiriki Mkutano huo kwa niaba ya Makatibu Wakuu wao.
Mkutano huo wa Makatibu umepitisha Ripoti waliyoijadili, ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri, ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahamoud Thabit Kombo ataongoza Ujumbe wa Tanzania kwa kushirikiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here