Rais Dkt.Samia aja na suluhu matumizi ya nishati ya mafuta nchini, awaapisha viongozi mbalimbali

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameelekeza kuwa maafisa na watumishi wa ofisi yake atakaoambatana nao katika safari zake za kikazi watatumia usafiri wa pamoja ili kubana matumizi ya nishati ya mafuta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Profesa Palamagamba John Aidan Kabudi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 08 Aprili, 2026.

“Nimeanza kwa upande wangu, kuanzia sasa, ninaposafiri, watendaji wa ofisi yangu nitakaoambatana nao watatumia usafiri wa pamoja wa mabasi madogo ili kupunguza matumizi ya mafuta na gharama za uendeshaji katika kipindi hiki,” amesema Rais Dkt. Samia.

Aidha, amezitaka Wizara na Taasisi nyingine za Serikali kuchukua hatua za kupunguza matumizi ya mafuta katika kipindi hiki.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Festo John Dugange kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 08 Aprili, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Gerson John Mdemu kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 08 Aprili, 2026.

Rais Dkt. Samia ameyasema hayo leo Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 08 Aprili, 2026.

Viongozi walioapishwa ni: Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu); Mhe. Dkt. Festo John Dugange kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI (Masuala ya Elimu); Mhe. Reuben Nhamanilo Kwagilwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira); na Mhe. Gerson Mdemu, Jaji wa Mahakama ya Rufani kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya kuwaapisha Viongozi Wateule, Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 08 Aprili, 2026.
Viongozi wateule wakiapa Kiapo cha Maadili kwenye hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 08 Aprili, 2026.

Rais Dkt. Samia amesema vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati vimeathiri nchi nyingi duniani, ikiwemo Tanzania, kutokana na kupanda kwa bei za mafuta na bidhaa.
Ameongeza kuwa, bei za mafuta zimefikia viwango vya juu katika baadhi ya nchi, hali iliyosababisha nchi hizo kupunguza shughuli za kiuchumi zinazotegemea matumizi ya Nishati ya Mafuta.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here