NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amewatakia Watanzania wote heri ya Sikukuu ya Pasaka iliyojaa furaha,amani na baraka tele.
Katika salamu zake kwa taifa leo Aprili 4,2026, RaisaDkt.Samia amewahimiza wananchi kutumia kipindi hiki cha maadhimisho ya ufufuko wa Bwana Yesu Kristo kutafakari na kuyaenzi mafundisho yake, hususan yale yanayohimiza huruma, upendo,msamaha na moyo wa kujitoa kwa ajili ya wengine.
Aidha, amesisitiza kuwa Sikukuu ya Pasaka iwe chachu ya kuimarisha amani, mshikamano na umoja wa kitaifa, misingi ambayo ni muhimu katika juhudi za kujenga taifa lenye fursa sawa kwa wote, ustawi wa jamii na maendeleo endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
