Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkubwa wa kitaifa utakaowakutanisha wauzaji chakula (Mamalishe na Babalishe) kutoka mikoa yote nchini.
Mkutano huo umepangwa kufanyika Aprili 11, 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na vyombo vya habari Aprili 4,2026 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wauzaji Chakula nchini kupitia Umoja wa Mamalishe na Babalishe Tanzania (UMALITA), Avijawa Omari, amesema kuwa wanaiomba Serikali kuwatambua rasmi kama kundi muhimu katika uchumi wa nchi.
Amesema kuwa utambuzi huo utawawezesha wanachama kupata mikopo, fursa za kiuchumi na kukuza ajira kwa vijana na wanawake nchini.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


















