ZANZIBAR-Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) kupitia Uwanja wake wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA) imerekodi ongezeko la idadi ya abiria na miruko ya ndege, jambo linaloashiria ukuaji endelevu wa sekta ya usafiri wa anga na ongezeko la mahitaji ya safari za ndege kwenda na kutoka Zanzibar.
Takwimu za mwezi Machi 2026 zinaonesha kuwa jumla ya abiria 187,407 walipitia katika uwanja huo, ikilinganishwa na abiria 174,654 walioripotiwa mwezi Machi 2025.
Hii inalingana na ongezeko la abiria 12,753, idadi inayoashiria kuimarika kwa safari za ndege na ongezeko la usafiri wa anga.
Kwa mujibu wa mgawanyo wa abiria, idadi ya wasafiri wa ndani imeongezeka kutoka 64,887 mwezi Machi 2025 hadi kufikia 74,791 mwezi Machi 2026.
Vilevile, abiria wa kimataifa wameongezeka kutoka 109,767 hadi 112,616 katika kipindi hicho.
Aidha, uwanja wa ndege wa AAKIA umeendelea kushuhudia ongezeko la miruko ya ndege, ambapo jumla ya miruko 4,838 iliripotiwa mwezi Machi 2026, ikilinganishwa na miruko 4,549 ya mwezi Machi 2025, sawa na ongezeko la miruko 289.
Ongezeko hili la shughuli za usafiri wa anga linachangia jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhakikisha viwango vya kimataifa vya usalama wa anga vinadumishwa.
Hii inajumuisha kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege, kuimarisha mifumo ya ukaguzi, na kuongeza uwezo wa rasilimali watu wanaohusika na masuala ya usalama wa anga.
Mafanikio haya yanatokana na uongozi unaoacha alama chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ambaye ameweka kipaumbele kikubwa katika uwekezaji,kuboresha huduma, usalama na ufanisi wa viwanja vya ndege vya Zanzibar, ili sekta ya usafiri wa anga iwe chachu ya ukuaji wa uchumi na utalii.
Mafanikio haya yanatokana na uongozi unaoacha alama chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ambaye ameweka kipaumbele kikubwa katika uwekezaji,kuboresha huduma, usalama na ufanisi wa viwanja vya ndege vya Zanzibar, ili sekta ya usafiri wa anga iwe chachu ya ukuaji wa uchumi na utalii.Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar imethibitisha kwamba,ongezeko la abiria na miruko ya ndege ni ishara ya imani iliyoongezeka kutoka kwa wasafiri wa ndani na kimataifa, huku ikiwa ni mwendelezo wa juhudi za Serikali katika kuhakikisha Zanzibar inabaki kuwa kitovu cha usafiri wa anga katika kanda ya Afrika Mashariki.
