Serikali yaanza rasmi kuimarisha Sekta ya Viwanda nchini

DODOMA-Serikali imeanza rasmi hatua za kuimarisha sekta ya viwanda nchini kwa kuzindua programu ya uhamasishaji kuhusu utekelezaji wa Kanuni za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) za uunganishaji na uzalishaji wa bidhaa za mwaka 2025, hatua inayotarajiwa kuongeza mnyonyoro wa thamani wa bidhaa, uzalishaji wa bidhaa na upatikanaji wa masoko ndani ya Jumuiya na hatimaye kukuza uchumi wa viwanda badala ya kutegemea kuagiza bidhaa kutoka nje.
Programu hiyo ilizinduliwa rasmi Machi 31, 2026 katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square jijini Dodoma, ikiwakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi, pamoja na waunganishaji na wazalishaji wa magari, pikipiki na bajaji kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumza na Wadau hao, Naibu Katibu Mkuu, Anayeshughulikia Masuala ya Uchumi, Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, wakati akifungua programu hiyo, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba, alieleza kuwa kanuni hizo ni nyenzo muhimu ya kimkakati itakayosaidia kuweka mfumo wa pamoja wa kikanda katika kusimamia shughuli za uunganishaji na utengenezaji wa bidhaa ndani ya nchi wanachama wa EAC.
Alieleza kuwa utekelezaji wa kanuni hizo utachochea maendeleo ya viwanda katika kuongeza mnyororo ya thamani ya bidhaa, kuimarisha ushindani wa viwanda vya ndani na kuweka mazingira thabiti na yenye uhakika kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika sekta ya uzalishaji.

Kwa mujibu wa Bw. Mwandumbya, Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa EAC zinazotekeleza Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya mwaka 2004 chini ya Itifaki ya Umoja wa Forodha, ambapo jitihada za awali zilianza mwaka 2013 kwa kuweka masharti ya uzalishaji wa ndani wa baadhi ya vifaa vinavyotumika kuunganisha pikipiki.

“Masharti hayo yalihusisha ulazima wa kutengeneza baadhi ya vipuri ndani ya Jumuiya, ikiwemo fremu kuu, siti, rimu za magurudumu pamoja na mifumo ya breki. Hata hivyo, utekelezaji wake uliendelea kuahirishwa mara kadhaa ili kutoa fursa kwa wazalishaji kujiandaa na kuwekeza katika uzalishaji wa ndani,"alifafanua Bw. Mwandumbya.

Alisema, hali hiyo ilisababisha kuibuka kwa hitaji la kuwa na mfumo wa pamoja wa kikanda utakaoratibu kwa ufanisi shughuli za uunganishaji na utengenezaji wa bidhaa, hatua iliyofikiwa mwaka 2024 baada ya nchi wanachama wa EAC kukubaliana kuanzisha Kanuni za Uunganishaji na Utengenezaji wa Bidhaa za Jumuiya ya Afrika Mashariki za mwaka 2025 (The EAC Assembling and Manufacturing of Products Regulations, 2025) ambapo Utekelezaji wake unatarajiwa kuanza rasmi ifikapo tarehe 01 Julai 2026.
Lengo la kanuni hizo ni kutoa mwongozo wa pamoja ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wa utaratibu wa uanzishaji na usimamizi wa skimu (scheme) za uunganishaji na uzalishaji wa bidhaa hususan vyombo vya moto ndani ya nchi wanachama ili kuangalia namna ya utoaji wa unafuu wa ushuru wa forodha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here