Waziri Dkt.Akwilapo akutana na Mtendaji Mkuu wa Shelter Afrique

NAIROBI-Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dkt.Leonard Akwilapo amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shelter Afrique, Bw.Thierno-Habib Hann jijini Nairobi, nchini Kenya.
Viongozi hao wawili wamekutana pembezoni mwa Kongamano la Miji Afrika (2nd African Urban Forum) lililofanyika kuanzia Aprili 8 hadi 10, 2026 nchini Kenya, na kukutanisha mataifa mbalimbali Barani Afrika kwa lengo la kubadilishana uzoefu na suluhisho bunifu katika kukabiliana na changamoto za maendeleo ya miji na makazi.
Dkt.Akwilapo na Bw.Thierno-Habib Hann katika kikao chao walijadili masuala mbambali yanayohusu uimarishaji wa upatikanaji wa makazi nafuu kwa wananchi pamoja na ushirikiano kati ya serikali na taasisi za kifedha katika kufanikisha azma hiyo.
Shelter Afrique ni taasisi ya kifedha ya kimataifa inayolenga kusaidia maendeleo ya makazi barani Afrika, huku makao makuu yake makuu yakiwa jijini Nairobi nchini Kenya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here