Waziri Kabudi ateta na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola

DAR-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amekutana na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Lazarus Chakwera jijini Dar Es Salaam Aprili 09, 2026.
Mjumbe Maalum huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo atakutana na wadau mbalimbali jijini Dar Es Salaam, Dodoma na Zanzibar.
Wakati wa ziara hiyo ambayo itahimishwa Aprili 16, 2026. Mhe. Chakwera amepangiwa miadi ya kukutana na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, asasi za kiraia na viongozi wastaafu.
Mhe. Chakwera aliwasili nchini Aprili 08, 2026 na kupokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe na alianza ratiba yake kwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo Aprili 09, 2026 jijini Dar EsSalaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here