Waziri wa Fedha ateta na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika

WASHINGTON D.C-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Zarau Wendeline Kibwe, katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, pembezoni mwa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na IMF (2026 IMF/WBG Spring Meetings) inayoendelea jijini Washington D.C, ambapo wamejadiliana kuhusu ushiriki wa Tanzania katika mikutano hiyo iliyoanza rasmi leo tarehe 13-19, Aprili 2026.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Fedha na Mipango kutoka Ofisi ya Rais-Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Balozi Elsie Sia Kanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here