Waziri wa Fedha kuongoza ujumbe wa Tanzania mikutano ya Kipupwe ya Magavana wa Benki ya Dunia na IMF

WASHINGTON D.C-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amewasili nchini Marekani, ambapo anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Kipupwe ya Magavana wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), itakayoanza Jumatatu tarehe 13 – 19, 2026, Makao Makuu ya Taasisi hizo jijini Washington D.C.
Mhe. Balozi Omar, ambaye aliambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, alilakiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Balozi Elsie Sia Kanza, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles, Washington D.C.
Mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa ina umuhimu mkubwa kwa Tanzania ambayo inamiki hisa katika Taasisi hizo kwa sababu inahusiana moja kwa moja na maendeleo ya kiuchumi, sera za kifedha na ustawi wa jamii wa Taifa na ni jukwaa muhimu la kujenga ushirikiano wa kimataifa, pamoja na kupata rasilimali za maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here