Waziri wa Fedha,Balozi Omar ashiriki Mkutano wa AfG1 wa IMF

WASHINGTON D.C-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ambaye pia ni Gavana wa Bodi ya Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, ameshiriki Mkutano wa nchi za Kundi la Kwanza za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency) wa Shirika hilo, uliofanyika katika Ofisi za Shirika hilo jijini Washington D.C, nchini Marekani, akiwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, katika mikutano inayoendelea ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, jijini humo.
Mkutano huo ulijadili Ripoti ya Muda ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Afrika kwa mwaka 2026, na namna ya Kukabiliana na Changamoto za Sekta ya Nje katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara (SSA) kwa kutumia Mfumo Jumuishi wa Sera wa IMF (IPF).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here