ACBF kuwajengea uwezo wataalamu wa Tanzania kwa kuakisi Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050

WASHINGTON D.C-Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ameongoza ujumbe wa wataalamu wa Tanzania katika kikao na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Kujenga Uwezo Afrika (The African Capacity Building Foundation-ACBF), Bw. Mamadou Biteye, uliofanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Washington D.C nchini Marekani, pembezoni mwa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na IMF (2026 IMF/WBG Spring Meetings) inayofanyika, Jijini humo, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya kuwajengea uwezo wataalamu nchini katika maeneo mbalimbali ya kipaumbele.
Dkt. Mwamba alitoa wito kwa taasisi hiyo kuanza kuwajengea uwezo wataalamu nchini Tanzania ambazo zitaakisi na kuendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, ili kupata ufanisi zaidi na matokeo katika kutekeleza Dira hiyo.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Bw. Sosthenes Kewe, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sheria, Wizara ya Fedha, Bi. Zawadi Maginga, Meneja wa Uchumi-Jumla kutoka Tume ya Taifa ya Mipango, Bi. Angela Uforo Shayo, na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here