DAR-Maji ya kimataifa ni moja ya rasilimali inayoleta amani katika nchi mbalimbali zinazonufaika na wananchi wake.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ( Mb) akifungua kikao cha 13 cha Baraza la Mawaziri la Kamisheni ya Bonde la Mto Zambezi (ZAMCOM) jijini Dar es salaam amesema maji hayana mpaka na yanakusanya watu kwa maendeleo yao.Mhe. Aweso ambaye katika mkutano huo ni Mwenyekiti ameainisha kuwa umoja wa wananchi na nchi walizopo umeletwa na maji ya kimataifa, maji yanayovuka mipaka ya nchi zao.
Amesema ni muhimu kuwa na rasilimali za kutosha ili kuleta maendeleo na wananchi wanashirikishwa kutunza rasilimali za maji ili kuleta maendeleo katika sekta nyingine za uchumi.
Mhe. Aweso amesisitiza kwa wajumbe wa mkutano huo kuwa maji ni muhimu na yanahitajika kuleta maendeleo kwa wananchi.










