DODOMA-Baraza la Taifa la Huduma Jumuishi za Fedha, likiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba, limefanya kikao chake cha 18 leo, tarehe 20 Mei 2026, katika ofisi za BoT jijini Dodoma.
Baraza hilo, lenye wajumbe 29 kutoka serikalini na sekta binafsi, limejadili mikakati mbalimbali inayolenga kuimarisha upatikanaji na matumizi ya huduma rasmi za fedha kwa wananchi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza ujumuishaji wa kifedha nchini.









