NA DIRAMAKINI
BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko kwenye kitengo chake cha Habari na Mawasiliano.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 14,2026 na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB),Cornel Barnabas.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Yahaya Abushe ameteuliwa kuwa Kaimu Ofisa Habari akichukua nafasi ya Karim Boimanda ambaye atapangiwa majukumu mengine na uteuzi huo unaanza mara moja.

