BoT yaongeza ukwasi katika Soko la Fedha za Kigeni, yaingiza dola milioni 20

NA GODFREY NNKO

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeshiriki katika Soko la Jumla la Fedha za Kigeni (IFEM) na kuuza dola milioni 20 za Marekani kupitia mnada wa ushindani.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 26,2026 na Kurugenzi ya Masoko ya Fedha ya BoT.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,ushiriki wa BoT ni kwa majibu wa Sera yake ya ushiriki katika Soko la Fedha za Kigeni ya Mwaka 2023.

BoT kupitia mnada huo imeuza dola hizo kwa kiwango cha wastani cha kubadilisha fedha za kigeni cha Shilingi 2,619.31 kwa dola moja ya Marekani.

Lengo la mnada huo ni kuongeza ukwasi katika soko la fedha za kigeni ambapo benki 21 zimeshiriki na zikashinda zote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here