Makatibu Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanaosimamia masuala ya mtangamano wamekutana katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya Mkutano Maalumu wa 60 wa Baraza la Mawaziri la EAC unaotarajiwa kufanyika tarehe 22 Mei 2026.
Kikao hicho cha Makatibu Wakuu kimepokea, kujadili na kupendekeza rasimu ya mapendekezo ya bajeti ya Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ambayo itawasilishwa katika Mkutano Maalumu wa Mawaziri kwa ajili ya idhini.Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Stephen Patrick Mbundi, alisisitiza umuhimu wa mkutano huo, akieleza kuwa kupitishwa kwa mapendekezo hayo ya bajeti kutasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekretarieti na taasisi zake, ikiwemo uhaba wa watumishi pamoja na ulipaji wa madeni ya watoa huduma.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


















