■Yaongoza Bara la Afrika, ikifuatiwa na Kigogo wa zamani Morocco (#9);
■Majirani zetu Afrika Mashariki Hawakuambulia japo Top 20 Duniani;
■Mwaka 2025 Watalii 5.9 Milioni Waliacha Tanzania Sh11.4 Trilioni;
■Profesa Kideghesho Apongeza, Ashauri Mikakati zaidi
Na Derek K. Murusuri
DUNIA inapozungumzia utalii kwa sasa, macho yote yameelekezwa Mashariki mwa Afrika. Chini ya uongozi wa "Mhifadhi na Muongoza Watalii Namba Moja," Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, sekta ya maliasili na utalii nchini Tanzania imevuka mipaka ya kawaida na kuingia katika vitabu vya rekodi duniani.
Kama ilivyobainishwa katika hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2026/2027, iliyowasilishwa bungeni leo tarehe 15 Mei, 2026 na Waziri thabiti wa sekta hiyo, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, kwa sasa Tanzania inashikilia funguo za soko la utalii duniani.
Nafasi ya Tatu Duniani na Pongezi kwa "The Royal Tour" Moja ya mafanikio makubwa yaliyoustua ulimwengu, ni ripoti ya Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) ya Januari 2026.
Ripoti hiyo imeitangaza Tanzania kuwa nchi ya tatu duniani kwa soko la utalii, lililofanya vizuri zaidi katika matumizi ya fedha (best performing market by spending).
Katika mjadala wa bajeti hiyo, takriban Wabunge wote waliochangia wametambua na kutoa pongezi za dhati kwa kazi iliyotukuka ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan...



