Taharuki Uwanjani! Bondia Mtanzania Japhet apoteza dhidi ya Mnigeria baada ya mabomu ya machozi kulipuka

NA DIRAMAKINI

BONDIA Mtanzania Loren Japhet amepoteza pambano lake dhidi ya bondia mwenyeji wa Nigeria, Basiti Adebayo katika mpambano uliofanyika nchini humo usiku wa kuamkia leo.
Pambano hilo lilikumbwa na sintofahamu katika raundi ya nne baada ya kuripotiwa kuwepo kwa milipuko ya vilipuzi vinavyodhaniwa kuwa mabomu ya machozi ndani ya ukumbi wa mashindano.

Tukio hilo lilisababisha pambano kusimamishwa kwa takribani dakika 20 huku waandaaji wakisubiri hali ya hewa kutulia na mazingira kuwa salama kwa kuendelea na mashindano.

Baada ya hali kurejea kuwa shwari, pambano liliendelea hadi mwisho wake, ambapo majaji walimpa ushindi bondia wa Nigeria, Basiti Adebayo, kwa alama (pointi).

Matokeo hayo yanamfanya Japhet kupoteza pambano hilo licha ya kuonyesha ushindani mkali kabla na baada ya kusitishwa kwa muda.
Tukio la kusimamishwa kwa pambano kutokana na milipuko hiyo limeibua maswali kuhusu usalama wa waangalizi na wanamichezo katika mashindano hayo, huku wadau wakitarajia ufafanuzi zaidi kutoka kwa waandaaji wa tukio hilo. https://www.instagram.com/reel/DX0DeAmIwWC/?igsh=MXE3d2Q1NHQwdmZtYg==

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here