Tanzania na Marekani zaendeleza ushirikiano wa kimkakati katika sekta muhimu

DAR-Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Ellen Maduhu, amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Andrew Lentz, kuhusu kuimarisha ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na Marekani.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walijadili namna ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, huduma za kibalozi, biashara na uwekezaji, usalama, nishati pamoja na utekelezaji wa mipango ya kimkakati ya maendeleo.
Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie S. Kanza, ambaye alishiriki katika majadiliano yaliyolenga kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Aidha, pande zote mbili zilisisitiza dhamira yao ya kuendelea kushirikiana na kufanya mazungumzo yenye tija kwa manufaa ya mataifa hayo mawili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here