DODOMA-Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu amekutana na Ujumbe wa Wabunge kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Mazungumzo hayo yamejikita katika kuimarisha ushirikiano wa kibunge kati ya Tanzania na DRC, kubadilishana uzoefu kuhusu mifumo ya utendaji kazi wa mabunge ya nchi hizo mbili pamoja na kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya mataifa hayo mawili.
Pande zote mbili zimeangazia umuhimu wa kuendelea kudumisha undugu, ushirikiano wa kikanda na maendeleo ya pamoja kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na DRC.
Ujumbe wa DRC umeongozwa na Mbunge wa Bunge la Kitaifa, Mhe. Prof. Willy Buhini akiambatana na Balozi wa Tanzania nchini DRC, Mhe. Said Mshana na Balozi wa DRC nchini Tanzania.




