Wabunge waonyeshwa mwelekeo wa mkakati wa Gridi ya Maji ya Taifa na manufaa kwa wananchi

DODOMA-Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameshiriki katika semina kuhusu Mpango Mkakati wa Gridi ya Maji ya Taifa. Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Bunge wa Msekwa jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji,Mhandisi Mwajuma Waziri katika mada yake amesema, Gridi ya Maji ya Taifa ni mfumo wa kimkakati wa usambazaji maji kutoka kwenye vyanzo vya uhakika na kuyapeleka katika maeneo yenye uhaba wa maji nchini.
Ameongeza kuwa,hadi sasa Wizara ya Maji imekamilisha vipande vya mtandao wa Taifa wa maji ikiwamo kutoa maji ziwa Victoria kwenda mikoa ya Shinyanga, Tabora na Shelui katika mkoa wa Singida.

Waziri wa Maji,Mhe.Jumaa Aweso (Mb) akihitimisha mada amewaomba ushirikishwaji wa jamii na ushirikiano kwa wabunge wote ili kuhakikisha mpango mkakati wa Gridi ya Maji ya Taifa unafanikiwa ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya majisafi na salama na kuchochea ukuaji wa uchumi ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo (DIRA 2050).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here