Wanne wahukumiwa kunyongwa hadi kufa mkoani Katavi

KATAVI-Mahakama Kuu ya Mkoa wa Katavi imewatia hatiani na kuwahukumu watu wanne kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya mauaji ya kukusudia mtu mmoja huko katika kijiji cha Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi.
Waliohukumiwa katika kesi hiyo ya mauaji ni Mwalemi Luyangula (23) mkazi wa Usevya, Lucia Julius (34) mkazi wa Inyonga, Kashindye Ikandago (36) mkazi wa Inyonaga na Lusoloja Machiha (28) mkazi wa Sikonge.

Akisoma hukumu hiyo Mhe.Hakimu Mfawidhi Gwayi Sumaye amesema,washitakiwa walitenda kosa hilo Juni 01, 2024 huko katika kijiji cha Inyonga, Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi baada ya kumuua kwa makusudi mtu mmoja aitwaye Jilala Kanengo Nkola (48), mkazi wa Inyonga kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali (panga) sehemu mbalimbali za mwili wake akituhumiwa kuwa ni mshirikina katika kijiji hicho.

Kesi hiyo namba 577/2024 ilifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 08, 2024 na hukumu kutolewa Mei 18, 2026 ambapo Hakimu Mfawidhi amebainisha kuwa mahakama imejiridhisha pasiposhaka na ushahidi uliotolewa na mashaidi 19 kutoka upande wa Jamhuri na umetosha kuwatia hatiani watuhumiwa hao.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mfawidhi Sumary amesema washitakiwa hao walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 197 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2023 na kueleza adhabu hiyo imetolewa ili iwe fundisho kwa washitakiwa na jamii katika kukomesha vitendo vya kikatili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here