Watoto 22 Bunju wakingwa dhidi ya ukatili

DAR-Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia kwa Polisi Kata ya Bunju, Mkaguzi wa Polisi (INSP) Mwanamosi, limeendesha kampeni maalum ya kutoa elimu ya usalama kwa watoto 22, inayolenga kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwajengea uwezo wa kujilinda dhidi ya mbinu mpya za wahalifu.
Mafunzo hayo ya ana kwa ana yamefanyika Mei 30,2026, katika eneo la Sobibo lililopo Mtaa wa Bunju A, Wilaya ya Kawe jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya mkakati endelevu wa kusogeza misingi ya ushirikishwaji wa jamii kwa tabaka la watoto.

Aidha,katika mafunzo hayo, INSP Mwanamosi aliwatahadharisha watoto hao vikali kutokubali kupokea zawadi au peremende kutoka kwa watu wasiowafahamu, huku akiwataka kuvunja ukimya na kutoa taarifa mapema kwa wazazi au Polisi pindi wanapohisi kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia au kuona viashiria vyovyote vya hatari.

Mafunzo hayo yalihitimishwa kwa watoto hao kukumbushwa kuwa na nidhamu kwa wazazi, huku zoezi zima likiacha alama chanya ya ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii, huku kukiwa hakuna changamoto wala matishio yoyote yaliyojitokeza kwenye himaya hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here