Waziri Kombo apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Kenya nchini

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo, amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Konseli Mkuu wa Jamhuri ya Kenya nchini, Mhe. Mohamed Ramadhan Ruwange, katika kikao kifupi kilichofanyika kwenye Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kidiplomasia na kusisitiza dhamira yao ya kuendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kenya. Aidha, walikubaliana kuendeleza majadiliano ya pamoja katika kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza katika juhudi za kuimarisha ushirikiano na mahusiano kati ya mataifa hayo mawili.
Mhe. Kombo amempongeza Mheshimiwa Ruwange kwa uteuzi wake na amemuhakikishia ushirikiano wakati wote atakapokuwa anahudumu hapa nchini.

Naye Mhe. Balozi Ruwange ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano uliopo na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo katika sekta mbalimbali zikiwemo biashara, uwekezaji, usafiri wa anga, miundombinu na utalii.
Maeneo mengine ni kilimo, teknolojia ya habari na mawasiliano, ufugaji na uvuvi, elimu, nishati, ulinzi na usalama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here