Waziri wa Fedha aongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha Taasisi ya WaterAid

BRAZZAVILLE-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao na Ujumbe wa Taasisi ya WaterAid UK, ukiongozwa na Mkurugenzi wake Mtendaji wa Kanda ya Kusini mwa Afrika, Bw. Robert Kampala, Mkutano uliofanyika pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa 61 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Mkutano Mkuu wa 52 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (ADF), unaoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kintele, Jijini Brazzaville, katika Jamhuri ya Kongo.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na WaterAid UK zimeahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimkakati ili kuendeleza huduma endelevu za Maji, Usafi wa Mazingira, na Usafi wa Binafsi (WASH).
Ushirikiano huo unalenga kuimarisha mifumo ya kitaasisi, kutekeleza miradi, na kupanua uwekezaji unaohimili mabadiliko ya tabianchi ili kuongeza kasi ya maendeleo ya sekta hiyo.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ambaye pia ni Gavana Mbadala (Alternate Governor) wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kaimu Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, na Bw Robert Mtengule, ambapo kwa upande wa WaterAid UK, alikuwepo Mkurugenzi wa Pan Africa Advocacy, Dkt. Tanko Yussif Azzika na maafisa wengine wa Wizara ya Fedha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here