Aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Katesh hatiani kwa uhujumu uchumi

NA DIRAMAKINI

MAHAKAMA ya Wilaya ya Hanang' mkoani Manyara imemtia hatiani aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Katesh, Sensa Gidang’adi Machakwa baada ya kupatikana na hatia ya kosa la matumizi mabaya ya madaraka lililosababisha hasara kwa fedha za kijiji.
Hukumu hiyo imetolewa Juni 3,2026 katika shauri la uhujumu uchumi namba ECC No. 7732/2026, ambapo mshtakiwa alikiri kosa kupitia utaratibu wa makubaliano ya kukiri kosa (Plea Bargaining Agreement) yaliyofikiwa kati yake na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Mtendaji huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 31 cha PCCA Cap 329 R: E 2023 vikisomwa pamoja na aya ya 21 katika jedwali la kwanza na kifungu cha 57(1) na 60(2) vya Sheria ya Kudhibiti Uhujumu uchumi na Makosa ya Kupanga Sura 200 R: E 2023.

Machakwa alitumia vibaya madaraka yake kwa kushindwa kuwasilisha benki kiasi cha shilingi 800,000 zilizotokana na mapato ya ukodishaji wa shamba la kijiji, badala yake akazitumia fedha hizo kwa manufaa yake binafsi.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Wilaya ya Hanang', Mheshimiwa Ponella Illoni amesema, mahakama imeridhika na makubaliano yaliyofikiwa kati ya upande wa mashtaka na mshtakiwa, na hivyo kumtia hatiani kwa kosa hilo.

Mahakama imeamuru mshtakiwa kulipa fidia ya shilingi milioni moja katika akaunti ya muhanga pamoja na kuachiliwa kwa masharti ya kutotenda kosa lolote la jinai ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Aidha,kabla ya hukumu kutolewa, mshtakiwa alikuwa tayari amerejesha shilingi 500,000 katika akaunti ya Kijiji cha Katesh iliyopo Benki ya NMB.

Kiasi kilichobaki anatakiwa kukirejesha kabla ya Juni 25, 2026 kwa mujibu wa makubaliano ya plea bargaining yaliyosainiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here