Gavana Tutuba afanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Afreximbank

DAR-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki ya Afrika ya Uagizaji na Usafirishaji Nje ya Nchi (African Export-Import Bank-Afreximbank) ulioongozwa na Mkurugenzi Mstaafu wa Operesheni za Ukanda wa Afrika Mashariki wa Afreximbank, Bw. Kudakwashe Matereke.
Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kumtambulisha rasmi Mkurugenzi Mpya na Mkuu wa Misheni wa Afreximbank kwa Ukanda wa Afrika Mashariki, Bw. Humphrey Nwugo kwa uongozi wa BoT.
Bw. Nwugo amechukua nafasi ya Bw. Matereke ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi na Mkuu wa Misheni wa Afreximbank katika Ukanda wa Afrika Magharibi.
Aidha, mkutano huo ulijadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili katika kustawisha sekta ya fedha, biashara na uwekezaji nchini ambayo itachangia kufikiwa kwa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Mkutano huo ulifanyika tarehe 25 Juni 2026, katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here