DAR-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, tarehe 16 Juni 2026, alikutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Africa Media Group Limited (AMGL), Bw. Dennis Msacky. Kampuni hiyo inamiliki na kuendesha kituo cha televisheni cha Channel Ten pamoja na redio ya Magic FM.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walijadili fursa za ushirikiano kati ya BoT na AMGL katika kuimarisha utoaji wa elimu ya fedha, uchumi na huduma za kifedha kwa umma.
Lengo la ushirikiano huo ni kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya fedha na uchumi, kuendeleza ujumuishi wa kifedha, na kuchochea ukuaji wa uchumi wenye kasi na jumuishi.
Aidha, walisisitiza umuhimu wa vyombo vya habari katika kufikisha taarifa sahihi za kiuchumi kwa wananchi, hatua ambayo itachangia kufikiwa kwa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.






