Jukwaa la Uunganishaji Masoko lawakutanisha washiriki zaidi ya 200 Manyara

MANYARA-Zaidi ya washiriki 200 kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Manyara wamekutana katika Jukwaa la Uunganishaji wa Masoko lililoandaliwa na Hand in Hand Eastern Africa Tanzania kwa lengo la kuwaunganisha wazalishaji na wanunuzi ili kuwapatia fursa za masoko.Akizungumza katika jukwaa hilo lililofanyika Juni 19, 2026 katika Hoteli ya White Rose mkoani Manyara, Meneja wa Tawi la Hand in Hand Mkoa wa Manyara, Bw. Yona Ona, amesema upatikanaji wa masoko ni daraja muhimu kati ya uzalishaji na ongezeko la kipato kwa wananchi.
“Jukwaa hili ni daraja kati ya uzalishaji na kuongeza kipato kwa kuwa linawakutanisha wazalishaji na wanunuzi moja kwa moja,” amesema Bw. Ona.

Jukwaa hilo ni sehemu ya jitihada za Hand in Hand Eastern Africa Tanzania za kuwafungulia wanufaika wake fursa za masoko na kuwawezesha kuongeza kipato kupitia shughuli za kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here