Magazeti leo Juni 18,2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua Awamu ya Pili ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia itakayofanyika Juni 20, 2026 katika Viwanja vya Dole, Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari Juni 17, 2026 jijini Dodoma, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Juma Homera, amesema kuwa kampeni hiyo ni utekelezaji wa maono na maelekezo ya Rais Samia ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma za msaada wa kisheria na haki zao kwa wakati.

Amesema kuwa kampeni hiyo ilianzishwa baada ya Rais Samia kubaini kuwa wananchi wengi wanakosa haki zao kutokana na kutofahamu sheria na kushindwa kupata msaada wa kisheria wanapokumbana na changamoto mbalimbali za kisheria.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here