Rais Dkt.Mwinyi amteua Mansura Mosi Kassim kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua ndugu Mansura Mosi Kassim kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Baraza la Mapinduzi, uteuzi huo umeanza rasmi leo Juni 22,2026 ambapo kabla ya uteuzi huo, Mansura Mosi Kassim alikuwa akihudumu nafasi ya Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa,uteuzi huo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha utendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuendelea kusimamia utekelezaji wa majukumu ya serikali kwa ufanisi.

Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi mpya anatarajiwa kuapishwa katika hafla itakayofanyika Ikulu Zanzibar mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi siku ya Jumatano ya Juni 24,2026

Uteuzi wa Mansura Mosi Kassim unakua ni Mwanamke wa Pili kushika wadhifa huo mkubwa katika utendaji wa serikali Zanzibar ambapo mwanamke wa mwanzo kuwa katika nafasi hiyo alikuwa ni Mhandisi Balozi Zena Ahmed Said.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here