Mke wa Rais wa Singapore atembelea kituo kinachozalisha nguo za pamba jijini Dar es Salaam

DAR-Mke wa Rais wa Singapore, Mheshimiwa Mama Jane Ittogi Shanmugaratnam, ametembelea kituo cha uzalishaji nguo za pamba zinazotengenezwa kwa mikono Msasani jijini Dar es Salaam na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika katika eneo hilo.
Akiwa katika kituo hicho, Mheshimiwa Mama Jane Ittogi Shanmugaratnam alitembelea maeneo tofauti ya uzalishaji na kushuhudia hatua mbalimbali za uchakataji wa pamba hadi kutengeneza nguo zinazozingatia ubora wa hali ya juu na utunzaji wa mazingira.

Akiwa katika kituo hicho, alielezwa namna wafanyakazi wa kiwanda hicho wanavyotumia ujuzi wa jadi pamoja na teknolojia za kisasa kuzalisha bidhaa za pamba zinazokidhi mahitaji ya masoko ya ndani na kimataifa.
Mheshimiwa Mama Jane alionesha kufurahishwa na ubunifu, ustadi na juhudi zinazofanywa na watumishi wa kiwanda hicho kidogo na wanavyotumia malighafi za ndani na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa kimataifa unaolenga kukuza biashara, uwekezaji na maendeleo endelevu.
Rais wa Singapore, Mheshimiwa Tharman Shanmugaratnam na mwenza wake wako nchini kwa ziara ya siku tatu ya kitaifa ikilenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Singapore.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here