Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yawaita wananchi Wiki ya Utumishi wa Umma viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma

DODOMA-Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imewakaribisha wananchi kutembelea banda la ofisi hiyo katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma kuanzia Juni 16 hadi 23,2026.
Akizungumza katika Maadhimisho hayo Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. George Ngerema amewakaribisha wananchi kutembelea katika banda la Ofisi ili waweze kupata uelewa wa kina kuhusu masuala ya kisheria, majukumu ya Ofisi, na jinsi inavyosimamia maslahi ya taifa.

“Tunawakaribisha wananchi waweze kutembelea kwa wingi kwenye banda letu kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za kisheria tutatoa huduma hii kwa wiki nzima ni tunaitoa bure kabisa,”amesema Bw.Ngerema.
Aidha, Bw. Ngerema ameeleza kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayatumia maadhimisho hayo katika kusogeza huduma za serikali karibu na wananchi.

Amesema kuwa,Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inatoa huduma za Elimu ya Sheria, msaada wa kisheria, utatuzi wa migogoro na kushughulikia malalamiko.

Maadhmisho ya Wiki Utumishi wa Umma mwaka 2026 yanafanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Doodma, yameanza tarehe 16 na yataendelea hadi tarehe 23 Juni, 2026 yamebeba kauli mbiu isemayo “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here