GEITA-Shule ya Royal Family English Medium Primary School imeendelea kujijengea sifa kubwa baada ya kuibuka kinara kwa kushika nafasi ya kwanza katika Manispaa ya Geita kati ya shule 91 katika mtihani wa Moko ya Kanda ya Ziwa.
Shule hiyo yenye wanafunzi 77 wa darasa la saba walioshiriki mtihani huo wameonyesha kiwango cha juu cha ufaulu ambapo wanafunzi 76 wamepata wastani wa A na mwanafunzi mmoja pekee akipata wastani wa B.Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo Mkurugenzi wa shule Mhandisi Lazaro Philipo amesema mafanikio hayo ni matokeo ya ushirikiano mkubwa kati ya walimu, wazazi na wanafunzi.

