Serikali itaendelea kuvutia uwekezaji Sekta ya Madini-Waziri Mavunde

DODOMA-Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia na kuwezesha miradi zaidi ya madini nchini.
Mavunde ameyasema hayo baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Marvel Gold ya Australia, Timothy Strong, ambaye alifika kutoa taarifa ya maendeleo ya mradi wa uchimbaji wa dhahabu unaotarajiwa kuanzishwa katika Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara

Amesema Serikali imefurahishwa na kasi ya utekelezaji wa hatua za awali za mradi huo, ambao kwa sasa upo katika hatua ya uchorongaji baada ya kukamilisha utafiti wa awali kwa kutumia teknolojia ya ndege zisizo na rubani (drones).
“Tunapongeza wawekezaji kwa kasi wanayoionesha katika kuendeleza mradi huu muhimu. Serikali itaendelea kushirikiana nao kuhakikisha sekta ya madini inachangia kikamilifu katika uchumi wa taifa,” amesema Mavunde.

Kwa upande wake, Strong amesema kampuni hiyo imeipongeza Serikali ya Tanzania kwa mazingira rafiki ya uwekezaji, akibainisha kuwa hatua ya awali ya uchorongaji inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Julai 2026.
Amesema, lengo la kampuni ni kuanza uzalishaji wa madini mara baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kiufundi na kisheria.

Mradi huo unatarajiwa kutoa ajira na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Wilaya ya Hanang na Mkoa wa Manyara kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here