TAKUKURU yaokoa Shilingi milioni 106 katika kesi ya uhujumu uchumi Mwanza

NA DIRAMAKINI

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi milioni 106 baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza kutoa hukumu dhidi ya viongozi wawili wa Chama cha Ushirika cha SUGECO wanaokabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi yaliyosababisha hasara kwa Serikali.
Hukumu hiyo imetolewa Juni 12, 2026 katika shauri la jinai namba ECC 13121/2026, linalowakabili Revocatus Vallery Kimario na Joseph Cyprian Masimba, ambao ni viongozi wa Chama cha Ushirika cha SUGECO kilichopo Mkoa wa Morogoro.

Katika uamuzi wake, mahakama iliwatia hatiani washtakiwa hao na kuwaamuru kurejesha kiasi cha Shilingi 106,000,000 katika akaunti ya TAKUKURU Wilaya ya Ukerewe, fedha ambazo mahakama ilibaini kuwa zilipotea kutokana na vitendo vilivyoisababishia Serikali hasara.

Mbali na amri hiyo ya kurejesha fedha, mahakama pia iliwatoza faini ya Shilingi 100,000 kila mmoja kwa makosa yaliyowakabili chini ya sheria za uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mahakamani, washtakiwa walikuwa wanakabiliwa na mashitaka ya kuisababishia Serikali hasara, kinyume na masharti ya Kifungu cha 57(1) pamoja na vifungu vya 62(1) na 62(2) vya Sheria ya Uhujumu Uchumi, Sura ya 200, Marejeo ya mwaka 2022.

Kesi hiyo ilisimamiwa na timu ya waendesha mashtaka wa TAKUKURU iliyojumuisha Moses Malewo, Cosmas Magesa na Nyamaindi Lisso, ambao waliwasilisha ushahidi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa Marley.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here