DODOMA-Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yaendelea kuwajengea uelewa wananchi juu ya masuala mbalimbali ya hali ya hewa kupitia maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Chinangali Park, Jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni,2026.
Maadhimisho hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 17 Juni 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete, na yanatarajiwa kufikia kilele chake tarehe 23 Juni 2026.
Katika maonesho hayo, wananchi wameendelea kukaribishwa kutembelea banda la TMA ili kutumia fursa hiyo kujifunza namna ya kuzitafsiri taarifa za hali ya hewa pamoja na matumizi sahihi kwa sekta husika ikiwemo kilimo, usafiri na uvuvi, hatua itakayosaidia kuongezeka kwa ufanisi katika shughuli za kimaendeleo.

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni: “Kuchochea uwajibikaji jumuishi kwa huduma endelevu.”
Tags
Habari
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Tanzania Meteorological Agency (TMA)
Utabiri wa Hali ya Hewa Tanzania
Wiki ya Utumishi wa Umma Tanzania


