Gereji zisiwe maficho ya wahalifu

DAR-Polisi Kata ya Viziwaziwa Mkaguzi wa Polisi Kondrad Kapinga akiwa na Sajini Peter Buyi wametoa elimu na kukagua gereji zilizopo katika Kata hiyo kwa lengo la kutoa Elimu ya kudhibiti uhalifu katika maeneo hayo.
Hayo yamesemwa Julai 6, 2026 katika gereji za Mgahi Mikongeni na Kwa Nestori Viziwa ziwa, ambapo wamiliki na wafanya kazi wa gereji hiyo wamekumbushwa kuepuka uhalifu kwa kuwaficha wahalifu katika maeneo hayo na kutokukununua vifaa toka kwa watu mikononi, kitendo ambacho kinaharibu taswira ya ofisi zao na kusababisha hasara kwa wateja wao.

Pamoja na elimu hiyo, pia walisisitizwa kuwa na tabia ya kuteketeza taili chakavu ili zisitumike kuchomwa au kuwa chanzo cha vuruguna kuteketeza vilipuzi vyote visivyo na matumizi ili kuepusha ajali za moto zisizotarajiwa na kuwataka kuwa na tabia ya kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa wakati katika maeneo yao ili kuepusha madhara kabla ya kutokea

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here