Kumbukumbu muhimu katika maisha ya Dogo Janja ambaye kwa sasa ni Diwani wa Ngarenaro

ARUSHA-Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Diwani wa Kata ya Ngarenaro jijini Arusha, Mheshimiwa Abdulaziz Abubakar Chende, maarufu kwa jina la kisanii Janjaro (zamani Dogo Janja), akimwonesha Rais picha aliyopiga naye Ikulu Dar es salaam mwaka 2010, walipokutana jijini Arusha jana.
Rais Mstaafu alikuwa mkoani humo kushiriki Mkutano wa Kamati ya Tuzo za Chakula Barani Afrika (Africa Food Prize Committee – AFP), uliofanyika Julai 23 hadi 24, 2026.

Dkt.Kikwete ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo inayofanya kazi chini ya Jukwaa la Mabadiliko ya Kijani Barani Afrika (AGRA), ambalo hutambua na kutoa tuzo kwa taasisi na watu binafsi waliotoa mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya kilimo na usalama wa chakula barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here