Magazeti leo Julai 12,2026

Mawaziri wa Nishati kutoka nchi wanachama wa Soko la Pamoja la Nishati Mashariki mwa Afrika (Eastern Africa Power Pool-EAPP) wameazimia kuharakisha utekelezaji wa soko la pamoja la umeme ili kuimarisha upatikanaji wa nishati, kuongeza biashara ya umeme kati ya nchi wanachama na kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa umeme katika ukanda huo.
Azimio hilo limefikiwa wakati wa Mkutano wa 22 wa Baraza la Mawaziri wa EAPP uliofanyika Julai 9 hadi 10, 2026 jijini Addis Ababa, Ethiopia ambapo Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Nishati.

Mkutano huo uliwakutanisha Mawaziri wa Nishati, wakuu wa taasisi za umeme na wawakilishi wa sekta ya nishati kutoka nchi wanachama wa EAPP kujadili hatua za kuimarisha ushirikiano wa kikanda kupitia biashara ya umeme, uunganishaji wa gridi za taifa na matumizi bora ya rasilimali za nishati.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here