Madereva wanaosafirisha makaa ya mawe nchini wamehimizwa kuzingatia kikamilifu sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia usafirishaji wa kemikali na bidhaa hatarishi ili kulinda usalama wa wananchi, mazingira na mali, sambamba na kuhakikisha shughuli za usafirishaji zinafanyika kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa.
Wito huo umetolewa na Meneja wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Kusini, Dkt. Hadija Mwema wakati akifungua mafunzo ya usafirishaji salama wa kemikali yaliyowahusisha madereva wa malori yanayosafirisha makaa yamawe wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Meneja alisema kuwa pamoja na makaa ya mawe kuwa bidhaa muhimu katika shughuli za kiuchumi, usafirishaji wake unapaswa kufanyika kwa kuzingatia sheria na kanuni za Usimamizi na Udhibiti wa kemikali ilikuzuia ajali, uchafuzi wa mazingira na madhara yanayoweza kujitokeza wakati wausafirishaji.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo











