Mkitumia vivuko vya waenda miguu barabarani mtakuwa salama wakati wa kwenda na kurudi nyumbani

SONGWE-Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkumbukwa iliyopo Kata ya Isongole Wilaya ya Ileje mkoani Songwe wamepewa elimu ya usalama barabarani yenye lengo la kuwajengea uelewa wa namna sahihi ya kutumia barabara na kuvuka kwa usalama katika kivuko cha waenda kwa miguu (Zebra Crossing).
Elimu hiyo ilitolewa Julai 26, 2026 na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Ileje, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Krisbert Kapondo, alipokuwa akiwaongoza wanafunzi hao kuvuka barabara ya Ileje–Mpemba kupitia kivuko cha waenda kwa miguu (Zebra Crossing), ambapo eneo hilo kila siku ya Jumamosi huwa na shughuli kubwa za soko zinazowavutia wananchi kutoka nchi jirani ya Malawi, hali inayosababisha ongezeko la watumiaji wa barabara pamoja na vyombo vya moto ikiwemo pikipiki, magari ya mizigo na magari yanayobeba abiria.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, ASP Kapondo aliwataka wanafunzi hao kuzingatia alama na sheria za usalama barabarani kwa kuhakikisha wanatumia vivuko maalumu vya watembea kwa miguu na kujiridhisha kuwa ni salama kabla ya kuvuka barabara.

ASP Kapondo aliwakumbusha wanafunzi hao kuwa elimu hiyo ni muhimu katika kupunguza ajali za barabarani zinazoweza kuepukika, huku kikosi hicho kikiendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kwa makundi mbalimbali ya jamii, hususan wanafunzi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza na kuzuia ajali, kulinda maisha ya wananchi na kujenga utamaduni wa kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here