DODOMA-Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy leo Julai 30, 2026 jijini Dodoma amezungumza na Wajumbe wa Rural Energy Working Group, ambalo ni Jukwaa lililoundwa na REA likishirikisha Taasisi mbalimbali za Serikali ambao ni Wadau muhimu katika kusambaza Nishati Bora Vijijini.
Mhandisi Saidy amesema kuwa,jukwaa hilo ni muhimu sana katika kuratibu, kubadilishana taarifa na kuwa na mipango ya pamoja katika kusaidia utekelezaji wa miradi ya Wakala na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya nishati bora vijijini kwa wakati.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikao hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti wa REA, Mhandisi Jensen Mahavile amesema kuwa kundi hilo pia ni jukwaa muhimu kwa sababu linatoa ushauri pamoja na kutoa ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazotokea wakati wa utekelezaji wa miradi ya kusambaza nishati bora vijijini.








