Mwenyekiti wa Kitongoji cha Makiwaru B wilayani Siha hatiani kwa kupokea rushwa ya Shilingi 20,000

KILIMANJARO-Julai 2,2026 Mahakama ya Wilaya ya Siha mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo,Mhe.Elibahati Petro imemkuta na hatia mshtakiwa wa shauri la jinai namba 13773/2026,Bw.Ismael Siroiya Pallangyo ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Makiwaru B kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha.
Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kosa la kupokea hongo ya shilingi 20,000 kutoka kwa mwananchi ili asimfikishe kwenye vyombo vya sheria kwa kumshambulia askari mgambo.

Kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya mwaka 2023.

Mshtakiwa baada ya kutiwa hatiani aliomba kupunguziwa adhabu,ambapo Mahakama iliamuru mshtakiwa kulipa faini ya shilingi 500,000 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani.

Aidha,mshtakiwa amelipa faini ya shilingi 500,000 na kukatiwa stakabadhi ya Serikali na yupo huru.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here