RPC Safia Jongo awapongeza askari kwa kuimarisha ulinzi na usalama,asisitiza nidhamu na weledi

GEITA-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, SACP Safia Jongo, Julai 16, 2026, amefanya Baraza la Maafisa, Wakaguzi na Askari Polisi lililofanyika katika Ukumbi wa FFU Geita, ambapo amewapongeza askari kwa juhudi za kuendelea kulinda amani na kuimarisha ulinzi na usalama wa raia pamoja na mali zao katika Mkoa wa Geita.
Kamanda Jongo amesema kuwa hali ya usalama katika Mkoa wa Geita imeendelea kuwa shwari, huku akibainisha kuwa mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano mzuri kati ya Jeshi la Polisi na wananchi. Amesema ushirikiano huo, pamoja na uwajibikaji, weledi na kujituma kwa askari katika kutekeleza majukumu yao kwa uzalendo, umeendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika mkoa huo.
Kadhalika, amewataka Maafisa, Wakaguzi na Askari Polisi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Kauli Mbiu ya Jeshi la Polisi inayosema, "Nidhamu, Haki, Weledi na Uadilifu," ili kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi, kuongeza imani ya wananchi kwa Jeshi la Polisi, pamoja na kudumisha amani, utulivu na usalama katika Mkoa wa Geita.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here